قالب وردپرس افزونه وردپرس قالب فروشگاهی وردپرس قالب وردپرس قالب صحیفه
Joel Lwaga

Joel Lwaga

Utambulisho.

Joel Lwaga ni muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, muabudu halisi aliyeitwa kuleta Tumaini.
Pia ni mchumi, mwandishi wa nyimbo na mwalimu wa Sauti.

Historia Fupi.

Joel Lwaga hatofautiani na waimbaji kadha wa kadha ambao huweka wazi kuwa wameanza kuimba wakiwa na umri mdogo kabisa kwenye shule ya Jumapili ya watoto yaani “Sunday School” na baadaye kujiunga na kwaya ya vijana akiwa kama muimbaji na mwalimu wa kwaya hiyo wakati huo akiwa anasali katika dhehemu la Morovian kabla ya kuhamia dhehebu la kipentekoste laTanzania Assemblies of God (TAG) ambapo kwa mara ya kwanza alijiunga na kanisa la City Christian Center Upanga.

Kwa mujibu wa Joel Lwaga mwaka 2013 ndio ulikuwa mwaka wake wa upenyo ambapo alipata nafasi ya kuongoza sifa na kuabudu kwenye ibada kubwa ya AFLEWO (Africa Let’s Worship) pamoja na AFLEWO Mass Choir ya Dar es Salaam ibada ambayo hutokea mara moja kwa mwaka Afrika nzima.

Baada ya hapo, Joel alijiunga na kundi la Glorious Worship Team huku akiendelea kuhudumu kanisani kwake na ndani ya kundi la The Next Level team.

Akiwa GWT alifanikiwa kushiriki kwenye albam ya kundi hilo inayojulikana kama "Waweza" ambapo katika albam hiyo aliweza kutunga na kuongoza wimbo uliobeba alban “Waweza” na wimbo mwingine unaoitwa "Ameniona" kabla ya kuachana na kundi hilo.

Joel amesema alidumu kwenye kundi la GWT kwa miaka miwili na kuanza kuimba kama muimbaji binafsi na kuweka wazi kuwa hakutoka ndani ya kundi kwa hila wala ubaya wowote bali ni suala la majira, nyakati na maono.

Kuimba kama Muimbaji Binafsi

Kwa sasa Joel anaimba yeye mwenyewe na ameshafanya huduma sehemu nyingi ikiwemo jijini Mbeya ambapo alimalizia masomo yake, lakini pia amepata mialiko mingi na kuhudumu kwenye majiji ya Arusha, Mwanza na Dar es salaam.

Mapema mwaka jana, Joel Lwanga alitoa Album yake kama muimbaji binafsi  SITABAKI KAMA NILIVYO ambao umempa umaarufu zaidi,  Joel ameeleza kuwa lengo kubwa la nyiimbo hizo  ni kujitambulisha yeye kana Muimbaji Binafsi na si kwenye Makundi tu kama watu walivyokuwa wamemzoea.
Album yake ya SITABAKI KAMA NILIVYO inapatikana YouTube kwa baadhi ya nyimbo lakini unaweza download nyimbo zake kupitia boomplay.

KUIMBA KAMA MUIMBAJI BINAFSI

Contacts
Phone# +255 715 747 597
Instagram- @joellwaga_official
Facebook- @Joel Lwaga.

Music